Shirika la habari la Ghana (Ghana News Agency) limeripoti kuwa warsha hiyo iliyoanza tarehe 24 Disemba ilisimamiwa na Muungano wa Jumuiya za Wanawake wa Kiislamu wa Ghana (FOMWAG) ukishirikiana na kitengo cha vijana cha jumuiya hiyo.
Lengo la warsha hiyo limetajwa kuwa ni kuwafunza wanawake wa Kiislamu jinsi ya kufikia mafanikio ya mtu binafsi na ya kijamii na kuhamasisha suala la kujifunza elimu mbalimbali hususan maarifa ya Kiislamu.
Mwenyekiti wa Muungano wa Jumuiya za Wanawake wa Kiislamu wa Ghana (FOMWAG) Bi Fatima Sulaiman amesema kuwa warsha hiyo imefanyika kwa mara ya kumi sasa nchini Ghana na kwamba mafunzo yake yamekuwa na mafanikio makubwa ikilinganishwa na ilpofanyika mwaka wa kwanza.
Kwa upande wake afisa anayeshughulikia masuala ya fedha wa jumuiya hiyo amewataka vijana wa kike wa Kiislamu kutumia vyema wakati wao na kuwahimiza suala la kutafuta elimu na maarifa kwa ajili ya kuweza kufikia malengo yao maishani.
Amesema vijana wengi hupoteza wakati wao mwingi wakitazama vipindi vya televisheni ambavyo vingi huwa na mafundisho yanayokwenda kinyume na thamani za Kiislamu. Amesisitiza kuwa badala ya kupoteza wakati katika mambo kama hayo vijana wa kiislamu wanapaswa kufanya juhudi za kutafuta elimu na maarifa ya Kiislamu. 718814