Kituo cha habari cha “Palestine.info” kimeripoti kuwa katika mwezi uliopita wa Disemba Wapalestina 13 wakiwemo mabarobaro 9 walitiwa nguvuni na askari wa Israel katika eneo la Silwan katika mji wa Baitul Muqaddas.
Wapalestina hao wanasema kuwa walipigwa na kuvunjiwa heshima na askari magereza wa Israel na kwamba mmoja wao alilazimishwa kukanyaga maandishi ya Kiebrania ambayo hakujua maana yake.
Wapalestina 8 akiwemo mpiga picha na mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitano walipigwa risasi na askari wa utawala katili wa Israel katika mwezi uliopita kwenye eneo hilo la Silwan katika mapigano ya askari jeshi wa Israel na vijana wa Kipalestina.
Mapigano hayo yalianza baada ya maafisa wa Israel kutangaza kwamba wana nia ya kufukuza familia 28 kutoka katika makao yao katika eneo la Silwan.
Nyumba nyingine tano za raia wa Palestina ziliharibiwa na askari katili wa Israel katika maeneo mengine ya Baitul Muqaddas. 723557