IQNA

Maulama wa Kisuni wa Iraq waharamisha mashambulio dhidi ya wafuasi wa dini nyinginezo

11:45 - January 06, 2011
Habari ID: 2059840
Maulama wa Kisuni wa Iraq wametoa fatuwa wakiharamisha mashambulio dhidi ya wafuasi wa dini nyinginezo katika nchi za Kiislamu na kusisitiza juu ya udharura wa kuishi pamoja kwa amani Waislamu na wafuasi wa dini hizo.
Baraza Kuu la Fatuwa la Ahlu Suna la Iraq lilitoa taarifa hiyo hapo jana Jumatano. Taarifa hiyo imesema kuwa, kwa mujibu wa Qur'ani Tukufu na viongozi wa kidini, uchokozi, kuua na kukosewa heshima maeneo ya ibada ya wafuasi wa dini nyinginezo katika nchi za Kiislamu ni jambo linaloharamishwa na kwamba kwa msingi huo baraza hilo limeharamisha kila aina ya tishio dhidi ya maisha na mali ya wasiokuwa Waislamu katika nchi za Kiislamu.
Fatuwa hiyo inawataka Waislamu kuishi pamoja kwa amani, udugu na upendo na ndugu zao Wakristo kama yanavyosema mafundisho ya Kiislamu.
Mashambulio ya kigaidi dhidi ya Wakristo yameongezeka sana katika siku za hivi karibuni katika nchi za Iraq na Misri. 725234
captcha