IQNA

Makongamano la 'Ushirikiano kati ya Dini na Kunufaika na Vyombo vya Habari' kufanyika Uswisi

13:20 - January 12, 2011
Habari ID: 2063470
Baraza Kuu la Waislamu la Uswisi lina mpango wa kuandaa mwezi huu mikutano na mawarsha kadhaa ya masomo kuhusu 'Ushirikiano kati ya Dini na Kunufaika na Vyombo vya Habari' huko Geneva.
Idara ya Uhusiano wa Umma wa baraza hilo ndiyo iliyopewa jukumu la kuandaa mikutano na mawarasha hayo.
Mikutano na mawarsha hayo yatawafundisha vijana wa Kiislamu njia za kutumia vyombo vya habari katika kukabiliana na picha mbovu inayoenezwa katika nchi za Ulaya na Magharibi na vyombo vya nchi hizo kuhusiana na Uislamu.
Shughuli za magazeti na majarida, mbinu tofauti zinazotumika katika uandishi wa magazeti na majarida kwa ajili ya kupambana na Uislamu, mafunzo ya mbinu za uzalishaji vipindi vya televisheni, redio, magazeti na intaneti, njia za kupunguza chuki dhidi ya Uislamu na kujishughulisha Waislamu na masuala ya kimataifa yanayohusu Uislamu ni masuala mengine yanayotarajiwa kujadiliwa katika mkutano na makongamano hayo. 728899
captcha