IQNA

Rais wa Iraq atoa msaada wa dinari milioni 10 kwa ajili ya ukarabati wa haram ya Imam Ali (as)

14:11 - January 16, 2011
Habari ID: 2065363
Rais Jalal Talabani wa Iraq ametoa msaada wa dinari milioni 10 kwa ajili ya kusaidia ukarabati wa haram ya Imam Ali bin Abi Twalib (as).
Ijumaa iliyopita Rais Talabani aliutembelea mji mtakatifu wa Najaf kwa lengo la kuonana na kuzungumza na wanazuoni wa Kishia wa mji huo na hasa Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Sistani. Baada ya kuonana na mwanazuoni huyo mashuhuri, Rais Talabani alizuru haram ya Imam Ali (as) na kutoa msaada uliotajwa kwa ajili ya ukarabati wa haram hiyo. Rais Talabani alisifu juhudi zinazofanywa kwa ajili ya kupanua haram hiyo.
Katika mazungumzo yake na Rais Talabani, Ayatullah Sistani alisisitiza kupatiwa huduma bora wananchi wa Iraq, mapambano dhidi ya ufisadi wa kiidara na kutekelezwa uadilifu nchini. Amesema serikali mpya ya Iraq imeonyesha azma thabiti ya kufikia malengo hayo na pia suala la kulindwa usalama wa Wakristo nchini humo.
Rais wa Iraq amesema kuwa Ayatullah Sistani amelaani vikali kulengwa Wakristo wa nchi hiyo na makundi ya kigaidi na kusema kuwa vitendo hivyo vya kigaidi vinatekelezwa kwa lengo la kuwatenganisha Wairaqi.
Akiwa mjini Najaf Rais Talabani pia ameonana na kuzungumza kwa nyakati tofauti na Maayatullah, Sayyid Muhammad Said Hakim, Sheikh Bashir Najafi, Muhammad Is'haq Fayadh na Sheikh Muhammad Ya'qubi. 730750
captcha