IQNA

Kozi za Qur'ani kwa familia za raia wa kigeni Qum

13:01 - January 31, 2011
Habari ID: 2072816
Taasisi ya Bibi Fatima SA ambayo inafungamana na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Moustafa imeandaa kozi za Qur'ani Tukufu kwa familia za wanachuo wa kidini wasiokuwa Wairani katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran miaka ya hivi karibuni.
Taasisi hiyo imekuwa ikiandaa kozi tokea mwaka 2005 kwa lengo la kuinua kiwango cha kielimu ya Qur'ani cha wake na watoto wa wanachuo wa kidini ili kuwapa uwezo wa kuhubiri Uislamu katika nchi zao.
Kozi hizo zinajumuisha kusoma Qur'ani, tajweed, ufahamu wa Qur'ani, tafsiri , akhlaqi na historia.
Taasisi hiyo pia imeandaa masomo maalumu kuhusu Ushia, Umahdi na kujitakasa mwanamke na Hijabu. Aidha washiriki wa kozi hizo walikutana na Marajii na vilevile waliandaa mashindano ya kusoma vitabu.
Taasisi hiyo ina benki ya programu za kompyuta pamoja na maktaba ya dijitali yenye kozi za Qur'ani na zaidi ya vitabu 2000 na CD 2000 za familia.
738373
captcha