Tovuti ya pr-usa imeripoti kuwa viongozi wa CAIR katika mji wa Tampa wametoa wito huo baada ya mtu mmoja asiyejulikana kumshambulia raia katika jimbo la Florida kwa sababu tu ya kuwa ni Muislamu.
Kwa mujibu wa ripoti ya polisi katika eneo la Pinellas, mhalifu huyo alimshambulia raia mwenzake siku kadhaa zilizopita katika mjadala wa kidini baada ya kutambua kwamba alikuwa Muislamu.
Mkurugenzi wa Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uislamu katika mji wa Tampa amesema viongozi wa jimbo la Frorida na majimbo mengine ya Marekani wanapaswa kuanzisha mapambano ya kukabiliana na propaganda chafu dhidi ya Uislamu la sivyo raia Waislamu wataendelea kushambuliwa na kukabiliana na vitendo vya kikatili.
Ramzy Clark amesema CAIR inafuatilia kisheria vitendo vinavyohujumu Uislamu na mashambulizi yanayofanywa dhidi ya wafuasi wa dini hiyo nchini Marekani. Baraza la CAIR pia limewataka Waislamu na vituo vya Kiislamu kufuata maelezo yaliyotolewa kwenye tangazo la kulinda jamii ya Waislamu la baraza hilo.
Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uislamu (CAIR) ndiyo jumuiya kubwa zaidi ya kutetea haki za Waislamu nchini Marekani. 744433