IQNA

Juhudi za jumuiya za Kiislamu za Uholanzi za kuanzisha tena Redio ya Kiislamu

12:49 - February 12, 2011
Habari ID: 2079212
Jumuiya za Kiislamu za Uholanzi zimeanzisha mazungumzo na wakuu wa televisheni na redio ya nchi hiyo kwa madhumuni ya kuanzisha tena redio ya Kiislamu nchini humo.
Kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni, viongozi wa jumuiya hizo wanakaribia kupata kibali hicho kutoka kwa wakuu wa televisheni na idhaa ya Uholanzi kuhusu jambo hilo.
Redio ya Kiislamu ya Uholanzi ilifungwa tarehe Mosi Februari na Shirika la Televisheni na Idhaa ya Uholanzi, kutokana na hitilifu zilizozuka kati ya jumuiya hizo za Kiislamu na Akademia ya Kiislamu ya nchi hiyo, jambo lililoungwa mkono na Mhakama ya Amsterdam.
Viongozi wa shirika hilo wamesema kuwa wako tayari kufanya mazungumzo na jumuiya zilizotajwa za Kiislamu kwa madhumuni ya kutatua hitilafu hizo. 745946
captcha