IQNA

Rais wa Russia ataka kuzidishwa adhabu kwa wanaofanya uhasama dhidi ya dini

17:16 - February 15, 2011
Habari ID: 2081551
Rais Dmitry Medvedev wa Russia ametoa wito wa kuzidishwa adhabu kwa watenda jinai zinazohusiana na chuki na uhasama dhidi ya dini na kuchochea ghasia za kidini na kikabila.
Shirika la habari la Interfax limeripoti kuwa Rais Medvedev amewataka wendesha mashtaka, wakaguzi na majaji wa Russia kutoa adhabu kali zaidi kwa watu wanaotenda jinai zinazohusiana na uhasama dhidi ya dini.
Amesisitiza kuwa adhabu kali zinapaswa kutolewa kwa wahalifu ili kuweza kukabiliana na harakati zinazochochea chuki za kidini na kikabila.
Rais wa Russia amesema kutotekelezwa adhabu kali dhidi ya wahalifu ni miongoni mwa sababu za kuongezeka vilitendo vinavyopiga vita dini nchini humo. 748320

captcha