IQNA

Mtazamo usiopendelea madhehebu yoyote wa Ayatullah Khamenei una athari kubwa katika kuleta umoja

14:57 - March 01, 2011
Habari ID: 2088645
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran chini ya uongozi wa Ayatullahil Udhma Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran imefanya juhudi kubwa za kuwaunganisha Waislamu na mtazamo usiokuwa na ubaguzi wa kimadhehebu wa Kiongozi Muadhamu katika hotuba zake ambazo amekuwa akizitoa katika sehemu mbalimbali umekuwa na taathira kubwa katika kuimarisha umoja miongoni mwa Waislamu.
Hayo yamesemwa na Sheikh Khalid Abdul Wahhab al-Mulla, Mkuu wa Jumuiya ya Maulama wa Ahlu Sunna wa Kusini mwa Iraq ambaye pia ni mwanachama wa Muungano wa Kitaifa wa nchi hiyo, alipokuwa akizungumza na shirika la IQNA. Amesema katika hotuba zake za Swala ya Ijumaa na vikao mbalimbali Ayatullah Khamenei amekuwa akiwasihi Waislamu wote duniani kuzingatia umoja na mshikamano kati yao bila kujali madhehebu zao, jambo ambalo amesema limekuwa na athari kubwa katika kuwaunganisha Waislamu.
Amesema umoja hauna maana ya kuunganishwa madhehebu za Kiislamu bali unawataka Waislamu kuwa na mtazamo na msimamo mmoja kuhusiana na changamoto, matatizo na masuala mbalimbali yanayoukabili ulimwengu wa Kiislamu.
Huku akiashiria umuhimu wa kufanyika kila mwaka mkutano wa Wiki ya Umoja wa Kiislamu mjini Tehran na athari zake katika nchi za Kiislamu, Sheikh Khalid Abdul Wahhab al-Mulla amesisitiza kwamba anaamini kuwa mikutano hiyo imekuwa na nafasi muhimu katika kuwaunganisha wanazuoni wa Kiislamu katika pembe tofauti za dunia. 755526
captcha