Sayyid Muhammad Said ambaye alikuwa akizungumza katika televisheni ya Pakistan amesema mabadiliko hayawezi kutokea katika jamii ya nchi hiyo bila ya kufuatwa mafundisho ya Kiislamu na kuyaeneza katika jamii.
Amesema mafundisho ya Mtume Muhammad (saw) na Qur'ani Tukufu ni mwongozo usiokuwa na kifani na akasisitiza juu ya udharura wa kutumiwa na kuenezwa mtazamo wa dini ya Kiislamu katika nyanja mbalimbali za kijamii.
Vilevile amevitaka vyombo vya habari vya Pakistan kuchukua majukumu yake katika uwanja huo na kujenga ushirikiano kati ya dini mbalimbali.
Amesema kwa sasa kuna misikiti karibu elfu 6 nchini Marekani, jambo ambalo ni ishara ya kuenea Uislamu kwa kasi nchini humo na katika nchini nyingine za Magharibi. 757922