Muungano huo unajumuisha vyama vya al Wafaa al Islami, Harakati ya al Haq na Harakati ya Watu Huru wa Bahrain.
Vyama vya upinzani vya Bahrain nchi ambayo imekumbwa na maandamano makubwa ya wananchi kwa wiki kadhaa sasa wanaotaka kuondoka madarakani mfalme wa nchi hiyo, vimetangaza kuwa vitaunda muungano mpya kwa ajili ya kubadili mfumo wa utawala wa kifalme na kuelekea kwenye mfumo wa jamhuri.
Taarifa iliyotolewa na makundi hayo imesema muungano huo mpya utafanya jitihada za kuondoa mfumo wa sasa wa utawala mutlaki wa kifalme na kuanzisha utawala wa jamhuri.
Maelfu ya wananchi wa Bahrain walianza maandamano tarehe 14 Februari wakitaka kubadilishwa katiba ya nchi na kuondolewa madarakani utawala wa sasa wa nchi hiyo.
Watu kadhaa wameuawa kwa kupigwa risasi na askari usalama tangu maandamano hayo yaanze na mamia ya wengine wamejeruhiwa. 760873