IQNA

Baraza Kuu la Waislamu Ujerumani lavunjwa moyo na matamshi ya Waziri wa Mambo ya Ndani

16:31 - March 09, 2011
Habari ID: 2093320
Baraza Kuu la Waislamu wa Ujerumani limetangaza kwamba limevunjwa moyo na matamshi yanayohujumu Uislamu yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo Hans-Peter Friedrich ambaye amedai kuwa dini ya Uislamu si sehemu ya nchi ya Ujerumani katika mtazamo wa kihistoria.
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu wa Ujerumani Iman mazik ametangaza kuwa matamshi hayo ya Waziri mpya wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani yanapingana na yale yaliyotolewa na Rais Christian Wulff wa nchi hiyo akisema kuwa Waislamu ni sehemu ya jamii ya sasa ya Ujerumani.
Ameashiria pia nafasi na mchango wa Waislamu katika harakati ya tarjumi na kupeleka falsafa ya Ugiriki huko Ulaya na akasema taathira ya Uislamu na Waislamu nchini Ujerumani na barani Ulaya kwa ujumla haiwezi kukanushwa na Waislamu walikuwa na nafasi kubwa katika nchi za Ujerumani, Uhispania na kusini mwa Italia.
Kuhusu suala la kuchangwanywa Waislamu katika jamii ya Ujerumani Iman Mazik amesema mazungumzo yote yaliyofanyika kuhusu suala hilo si kamili na hayakuwa na natija. Amesisitiza kuwa kutokuwepo mazungumzo ya moja kwa moja kati ya wawakilishi rasmi wa serikali ya Ujerumani kama Waziri wa Mambo ya Ndani na wawakilishi wa jamii ya Waislamu wa Ujerumani kumekwamisha jitihada za kuwaunganisha Waislamu katika jamii. 760802



captcha