Shirika la habari la Trend limeripoti kuwa kongamano hilo linafanyika kwa kaulimbiu ya ustawi wa masoko ya rasilimali za Kiislamu nchini Kazakhsan na nchi za Urusi ya zamani.
Waziri Mkuu wa Kazakhstan Karim Masimov na Waziri wa Viwanda na Teknolojia wa nchi hiyo wameshiriki katika ufunguzi wa kongamano hilo.
Shakhsia mbalimbali wa taasisi za kimataifa kutoka Mashariki ya Kati, Ulaya, Asia na America wanashiriki katika kongamano hilo. 763435