Mafunzo hayo yataendeshwa katika msikiti wa Sunna ambao ni msikiti mkongwe zaidi katika mji huo na tayari walimu wa shule kadhaa za Kikatoliki wametangaza hamu yao ya kushiriki katika mafunzo hayo ili kuelewa misingi ya mafundisho ya Kiislamu. Walimu hao wanasema kuwa kuna uadharura wa kufahamu misingi hiyo kutokana na ukweli kwamba kuna wanafunzi wengi wa Kiislamu wanaosoma katika shule za Kikatoliki katika mji huo. Akizungumzia suala hilo, Rachid Sahri, Mkuu wa Taasisi ya Kiislamu ya mji wa Roubaix amesema kuwa mafunzo hayo yatachangia pakubwa katika kuimarisha utamaduni wa mazungumzo kati ya wafuasi wa dini na tamaduni tofauti nchini Ufaransa. 767876