IQNA

Kituo cha Kiislamu cha ‘Noor’ chafunguliwa Ethiopia

18:46 - April 09, 2011
Habari ID: 2102879
Kituo cha Kiislamu cha ‘Noor’ kimefunguliwa Ethiopia katika hafla iliyohudhuriwa na mwambata wa utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini humo pamoja na maimamu , wahubiri, waalimu na wanafunzi mjini Bulbula.
Akizungumza katika sherehe za ufunguzi wa kituo hicho, Imam wa Sala ya Ijumaa mjini humo aliashiria aya za Qurani Tukufu zinazohimiza umuhimi wa elimu na masomo. Ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuchukua hatua nzuri ya kufadhili kituo cha Kiislamu.
Akihutubi katika hafla hiyo, mwambata wa utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Ethiopia Mohsen Ashur amefafanua kuhusu aya katika Sura Nasr ya Qurani Tukufu kuhusu wanaosilimu.
Amesema kuna haja ya juhudu kufanyika kutumia fursa zilizopo za kuinua kiwango cha elimu ya wakaazi wa eneo hilo.
770559

captcha