IQNA

Hussein Ruyvaran:

Lengo la uvamizi wa Saudia nchini Bahrain ni kuwagombanisha Shia na Suni

12:42 - April 24, 2011
Habari ID: 2110929
Moja ya malengo makuu ya uvamizi wa Saudi Arabia nchini Bahrain ni kuwagonganisha pamoja Waislamu wa madhehebu za Shia na Suni na kuanzisha vita vya kimadhehebu.
Hayo yamesemwa na mtaalamu wa masuala ya Mashariki ya Kati Hussein Ruyvaran katika mahojiano yake na shirika la IQNA. Ameongeza kuwa sisitizo la Saudi Arabia kwamba wapinzani wote wa utawala wa kidikteta wa Bahrain ni Mashia, linakusudia kuchochea Waislamu wa madhehebu ya Suni hususan nchini Saudi Arabia dhidi ya wananchi wa Bahrain.
Amesema kuwa mgogoro wa Bahrain ni mapinduzi yanayowasirikisha wananchi karibu wote na utawala wa Manama umeamua kuomba msaada wa nchi kama Saudi Arabia na Imarati baada ya kushindwa kukabiliana na mapinduzi ya wananchi.
Hussein Ruyvaran amesema kuwa uingiliaji wa Saudia nchini Bahrain umekiuka sheria za kimataifa kwani mapambano ya wananchi kwa ajili ya kuainisha mustakbali wa nchi yao ni miongoni mwa haki za kimsingi za kimataifa. Amesema uvamizi wa Saudi Arabia na Imarati huko Bahraini umezidisha mgogoro wa nchi hiyo. 779350

captcha