Huku akiwapongeza Wakristo wa Lebanon kwa mnasaba wa sikuu ya Pasaka, Ayatullah Qabalan ameelezea matumaini yake kwamba wananchi wa Lebanon watatumia fursa hii ya kidini kwa ajili ya kuimarisha umoja na mshikamano wao. Ameendelea kusema kuwa ni matumaini yake kwamba wananchi wa Lebanon watatumia fursa hiyo kutekeleza vyema majukumu yao ya kidini ambayo yanawataka wote kuishi pamoja kwa amani mbali na mielekeo ya chuki na ubaguzi.
Vilevile amewataka waunde haraka serikali ya umoja wa kitaifa kwa ajili ya kupambana na njama za maadui wao. 780346