IQNA

Kikao cha viongozi wa Kiislamu na Kiyahudi wa Ufaransa kulalamikia ubaguzi

17:13 - May 09, 2011
Habari ID: 2119223
Viongozi wa Kiislamu na Kiyahudi wa Ufaransa jana Jumapili walifanya kikao huko Paris mji mkuu wa Ufaransa kwa shabaha ya kulalamikia siasa za ubaguzi zinazotekelezwa na serikali ya nchi hiyo dhidi ya baadhi ya jamii za nchi hiyo.
Kwa mujibu wa tovuti ya atlasinfo washiriki wa kikao hicho ambacho kiliandaliwa na Jumuiya ya Urafiki ya Uislamu na Uyahudi ya Ufaransa AJMF ambao pia walijumuisha wawakilishi wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC na Kituo cha Mayahudi wa Ufaransa, wamebainisha malalamiko yao kuhusiana na siasa za ubaguzi zinazotekelezwa na Chama cha Kitaifa cha Ufaransa FN dhidi ya Waislamu na Mayahudi wa nchi hiyo.
Washiriki wa kikao hicho wametangaza wazi kwamba Waislamu na Mayahudi wa nchi hiyo hawatakipigia kura chama hicho katika uchaguzi ujao wa rais wa mwaka 2012.
Waislamu na Mayahudi wa Uingereza pia wamepanga kufanya kikao kama hicho hii leo Jumatatu mjini London ambapo wanatazamiwa kusisitiza juu ya ulazima wa kuishi pamoja kwa amani wafuasi wa dini tofauti na vilevile kulindwa haki za kiraia za jamii za wahajiri wanaoishi katika nchi hiyo. 788390
captcha