Hayo yamesemwa na Sayyid Hassan Musawi Bahraini, mwanaharakati wa kisiasa wa Bahrain katika mazungumzo yake na IQNA. Amesema baada ya Februari 14 Aal Khalifa na Aal Saud waliingia katika kinamasi ambacho ni vigumu kuondoka ndani yake bali wanazidi kuzama katika kinamasi hicho kwa vitendo vya kuvunjia heshima Qur'ani na kuvunja misikiti na nyumba za ibada.
Sayyid Hassan Musawi ameashiria kuwa Marekani na Uingereza daima wamekuwa wakitekeleza siasa za kindumakuwili kuhusu masuala ya eneo la Mashariki ya Kati na kuongeza kuwa si jambo la kushangaza kuona siasa kama hizo kutoka nchi za kikoloni.
Ameashiria pia msimamo wa nchi za Kiarabu kuhusu harakati ya wananchi wa Bahrain na kusisitiza hadithi ya Mtume inayosema: Muislamu anayesikia sauti ya Muislamu mwenzake akiomba msaada kisha asimjibu huwa si Muislamu. Amesema Waislamu wanapaswa kusaidia Waislamu wenzao wanaoteseka na kudhulumiwa.
Vilevile ameitaka jamii ya kimataifa kuzidisha mashinikizo ya kuwatetea wananchi wa Bahrain na kusema kuwa mashinikizo hayo yatawalazimisha watawala madhalimu wa Bahrain kupunguza ukandamizaji dhidi ya wananchi na hatimaye mapinduzi ya wananchi hao yatapata ushindi. 789538