Kwa mujibu wa tovuti ya alitrah.info kitabu hicho chenye kurasa 96 kimeandikwa na Sheikh Nizari Hasan na kutarjumiwa na Hemed Lubumba (Abu Batuli) .
Kuhusu lengo la kuchapisha kitabu hicho, taasisi ya Al Itrah imesema kuwa suala la madhehebu lilianza kuzungumzwa na Mtukufu Mtume SAW mwenyewe katika hadithi zake tukufu: "Mayahudi walikuwa madhehebu sabini na tatu baada ya Nabii Musa AS, na Wakristo madhehebu sabini na mbili baada ya Nabii Isa AS, na Umma wangu huu utakuwa na madhehebu sabini na moja baada yangu, na (madhehebu) zote (zitaingia) motoni isipokuwa moja.”
Taasisi hiyo imeongeza kuwa kutokana na kauli hii ya Mtume SAW ni kwamba suala la madhehebu haliwezi kuepukika, lazima madhehebu zitakuwepo bali changamoto moja tu iliyoko katika kauli hii ni kwamba madhehebu zote hizo zitaingia motoni isipokuwa moja. Suala hapa sasa ni kufanya utafiti ili kujua ni madhehebu ipi hiyo itakayokuwa salama, na sio kugombana kwa jambo ambalo lilikwishatabiriwa na Bwana Mtume mwenyewe - na hiki ndicho alichofanya mwandishi wa kitabu hiki.
789899