IQNA

Kuundwa muungano wa kwanza wa wanamapinduzi wa Kiarabu mjini Cairo

12:22 - May 15, 2011
Habari ID: 2122352
Zakaria Abdul Aziz, mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Majaji wa Misri ametangaza habari ya kuundwa hivi karibuni muungano wa kwanza wa wanamapinduzi wa Kiarabu mjini Cairo kwa lengo la kuunga mkono mapinduzi ya wananchi katika nchi za Kiarabu.
Kwa mujibu wa tovuti ya egynews, Abdul Aziz amesema kuwa muungano huo utakuwa na wawakilishi kutoka nchi za Misri, Libya, Yemen, Iraq na Lebanon kwa madhumuni ya kufuatilia na kuratibu malengo ya mapinduzi ya Misri na mapinduzi ya nchi nyinginezo za Kiarabu. Amesema, wanamapinduzi wa Kiarabu tayari wanashauriana kisiasa kwa lengo la kutoa misaada ya kibinadamu na kuakisiwa vyema harakati za mapinduzi za wananchi wa Libya na Yemen ili kuwaondolea matatizo yanayowakabili yakiwemo ya uhaba wa dawa na bidhaa za chakula.
Abdul Aziz amesema kuwa muungano huo utaunda kamati maalumu ya kuratibu na kufuatilia malengo ya mapinduzi ya wananchi wa nchi za Kiarabu na kuwashawishi wayaunge mkono kwa dhati.
Kamati hiyo itakuwa na makao makuu yake mjini Cairo. 791328
captcha