IQNA

Ubaguzi wa serikali ya Saudia ndiyo sababu ya migawanyiko kati ya Shia na Suni

19:23 - May 16, 2011
Habari ID: 2123335
Mwanafikra wa Kishia wa Saudi Arabia Hashim Salman amesema kuwa ubaguzi unaofanywa na serkali ya nchi hiyo dhidi ya Waslamu wa madhehebu ya Shia ndio sababu kuu ya migawanyiko iliyopo kati ya Waislamu wa Shia na Suni huko mashariki mwa Saudia.
Hashim Salman ambaye pia ni imam wa msikiti wa Rasulul Aadham katika mji wenye Waislamu wengi wa madhehebu ya Shia wa Ihsaa mashariki mwa Saudi Arabia, amesema kuwa uhusiano baina ya Waislamu wa madhehebu za Shia na Suni umenyong'onyea mashariki mwa Saudia ilhali Waislamu hao wamekuwa wakiishi pamoja kwa amani kwa miaka mingi.
Sheikh Salman amewataka Waislamu wote wa mashariki mwa Saudia Shia kwa Suni, kujiepusha na mambo yote yanayosababisha hitilafu na mivutano na kuimarisha umoja na mshikamano wao.
Amesema serikali ya Saudi Arabia imekuwa ikipanda mbegu za hitilafu na fitina baina ya Waislamu kwa kuwabagua Mashia, kutoa nara za kimadhehebu na kusisitiza juu ya hitilafu za kimakundi kupitia vyombo vya mawasiliano ya umma. 792583


captcha