Wito wa kushiriki katika harakati hiyo ulitolewa katika mtandao wa kijamii wa Facebook. Wito huo uliwataka wakazi wote wa mji huo kutangaza mshikamano wao na Waislamu wenzao wa Bahrain na kulaani vitendo vya kuvunjiwa heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani na kuvunjwa misikiti vinavyofanywa na jeshi la utawala wa Aal Khalifa ukishirikiana na askari kutoka Saudi Arabia. kufuatia wito huo sauti za Allahu Akbar zilisikika jana usiku katika paa za nyumba za mji huo.
Mji wa al Awwamiyya wenye wakazi wengi wa madhehebu ya Shia huko mashariki mwa Saudi Arabia umekuwa ukishuhudia maandamano ya wananchi kwa miezi mitatu sasa ambao wanadai haki zao wa kijamii na kidini.793651