Vikao hivyo viliandaliwa na Kituo cha Tathmini ya Kijamii CADIS na Chuo cha Utafiti wa Juu wa Taaluma ya Kijamii cha Paris EHESS. Wasomi mbalimbali mashuhuri wakiwemo Daniel Joly, John Bowen, Nacira Guenif-Souilamas na Dounia Mouzar wameshiriki vilivyo kwenye vikao hivyo na kutoa mchango wao kuhusiana na matatizo yanayowakabili wanawake wa Kiislamu katika juhudi zao za kushirikishwa kwenye masuala mbalimbali ya kijamii na kisiasa katika nchi za Magharibi na hasa Ufaransa na Uingereza. 793027