IQNA

Misikiti ya kusini mwa Ufaransa yasusia uchaguzi wa Baraza Kuu la Waislamu

12:54 - May 21, 2011
Habari ID: 2125284
Asilimia 84 ya misikiti ya eneo la Rhône-Alpes kusini mwa Ufaransa imesusia uchaguzi wa Baraza Kuu la Waislamu nchini humo CFCM.
Kwa mujibu wa tovuti ya fr.zaman, misikiti hiyo imechukua hatua hiyo katika kulalamikia namna uchaguzi wa baraza hilo ulivyopangwa kufanyika mwezi ujao.
Akizungumzia suala hilo Izzu Deen Qaji mwakilishi wa baraza hilo katika eneo la Rhone-Alpes amesema kuwa kwa kuzingatia kwamba ni jumuiya za Kiislamu 16 tu ndizo zilizojiandikisha kushiriki kwenye uchaguzi huo kinyume na ilivyokuwa mwaka 2008 ambapo jumuiya 80 za eneo hilo la kusini mwa Ufaransa zilishiriki uchaguzi, kufanyika uchaguzi wa mwezi ujao katika eneo hilo hakutakuwa na maana. Amesema uchaguzi huo unapasa kuakhirishwa ili kuwapa fursa maafisa husika watazame upya mipango ya kuandaa uchaguzi huo. 794975
captcha