IQNA

Propaganda chafu za kuwatisha watu kuhusu Uislamu, mfano wa ubaguzi katika jamii ya Marekani

15:00 - May 25, 2011
Habari ID: 2128512
Mhadhiri wa masuala ya utamaduni katika Chuo Kikuu cha North Carolina amesema katika kuarifisha kitabu chake kipya alichokipa jina la “Kuwatisha Watu Kuhusu Uislamu: Vita vya Kiaidiolojia dhidi ya Uislamu” kwamba mwenendo wa kuuchafulia jina Uislamu ni mfano wa ubaguzi wa kimbari katika jamii ya Marekani.
Stephan Shihi amesema ubaguzi wa kimbari ni tabia iliyokuwepo kwa miaka mingi nchini Marekani kwa ajili ya kutekeleza siasa za ‘tenganisha utawale’.
Mhadhiri huyo wa chuo kikuu amesema propaganda chafu zinazofanywa katika nchi za Magharibi dhidi ya Uislamu na Waislamu ni fikra ya makundi yenye misimamo ya kufurutu ada nchini Marekani.
Sherehe ya uzinduzi wa kitabu cha“Kuwatisha Watu Kuhusu Uislamu: Vita vya Kiaidiolojia dhidi ya Uislamu” ambazo zimefanyika katika Chuo Kikuu cha North Carolina zimehudhuriwa na wanachuo wa chuo hicho na wawakilishi wa jumuiya za Kiislamu. 798338
captcha