Kituo cha habari cha MBC kimeripoti kuwa baada ya wimbi kubwa la malalamiko na ukosoaji wa wananchi wa Tunisia katika mtandao wa kijamii wa Facebook, mawakili watatu wa nchi hiyo waliwasilisha mashtaka mahakamani wakitakata kuchujwa mitandao yote inaokwenda kinyume na maadili na thamani za Kiislamu.
Lengo la hatua hiyo limetajwa kuwa ni kuzuia taathira mbaya za mitandao hiyo kwa fikra na maadili ya jamii.
Ripoti zinasema kuwa mitandao yenye mambo yanayokwenda kinyume na maadili na thamani za Kiislamu imeenea mno nchini Tunisia tangu baada ya kuondolewa vizuizi vya intaneti kufuatia mapinduzi yaliyouondoa madarakani utawala wa kidikteta wa Bin Ali. 800379