Kongamano la 'Maisha ya Kisiasa na Kijamii ya Imam Khomeini Mwenyezi Mungu amrehemu, litafanyika nchini Zimbabwe kwa mnasaba wa mwaka wa 22 tangu mwasisi huyo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aage dunia.
Mwandishi wa IQNA ameripoti kuwa kongamano hilo litafanyika Ijumaa tarehe 3 Juni katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Zimbabwe.
Mkuu wa Kitengo cha Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Charity Manyeruke, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislamu ya chuo hicho Ali Jonson, balizi wa Iran nchini Zimbabwe Pournajafi na Mwambata wa Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini humo Asadi Muwahhidi watahutubia kongamano hilo.
Kandokando na kongamano hilo kutakuwapo maonyesho ya vitabu na maandiko ya hayati Imam Ruhullah Khomeini, vitabu vinavyohusiana na sayansi ya Qur'ani na vitabu vingine vya kidini na maeneo ya Kiislamu nchini Iran.
Kikao kingine kama hicho pia kitafanyika katika Kituo cha Imam Khomeini katika mji wa Kaduma. 800912