IQNA

Kongamano la vijana wa Kiislamu wa Ufaransa lafanyika

15:54 - June 19, 2011
Habari ID: 2140484
Kongamano la saba la kila mwaka la vijana wa Ufaransa limepangwa kufanyika leo Jumapili tarehe 19 Juni katika jimbo la Bourgogne chini ya anwani ya 'Siku ya Masomo.'
Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Jumuiya ya Vijana wa Kiislamu wa Jimbo la Bourgogne linahudhuriwa na wanachuo bora, wavumbuzi na watafiti wa Kiislamu. Washiriki wa kongamano hilo watawasilisha utafiti na uvumbuzi wao walioufanya katika nyanja mbalimbali za kielimu, kiufundi na kidini.
Kushajiishwa vijana wa Kiislamu kufanya uvumbuzi na utafiti wa kielimu, kuarifishwa wavumbuzi na watafiti bora wa Kiislamu nchini Ufaransa na kubadilishana uzoefu kati ya washiriki wa kongamano hilo ni miongoni mwa malengo muhimu ya kufanyika kongamano hilo.
Ratiba nyingine za kongamano hilo ni pamoja na kutunukiwa zawadi vijana wa Kiislamu, kuandaliwa vikao vya kidini na kiutamaduni, maonyesho ya masuala ya Kiislamu na uvumbuzi wa Waislamu wa Ufaransa pamoja na kutolewa hotuba za wahadhiri na wanazuoni wa Kiislamu. 811005
captcha