Kituo cha Kiislamu cha Britani kumetangaza kuwa lengo la hafla hiyo ni kuwafanya watu wajue na kutambua utamaduni, itikadi, ada na desturi za Kiislamu na kukabiliana na propaganda zinazoichafulia jina dini ya Kiislamu.
Katika shughuli hiyo kutakuwa pia na maonyesho ya vitu mbalimbali ambapo watazamaji watapata fursa ya kujua mengi kuhusu Qur’ani Tukufu, Mtume Muhammad (saw) Nabii Ibrahim, Mussa, Issa na Mitume wengine wa Mwenyezi Mungu.
Maonyesho hayo pia yatakuwa na vitabu vya Kiislamu, chakula na mavazi ya Waislamu na kadhalika.
Kadhalika kutakuwa na programu makhsusi za burudani kwa ajili ya watoto na familia zao. 811764