IQNA

Baraza la Waislamu la Ufaransa, mwakilishi wa utamaduni wa Kiislamu nchini humo

14:26 - June 22, 2011
Habari ID: 2142431
Muhammad Musawi, Mkuu wa Baraza la Waislamu la Ufaransa amesema kuwa baraza hilo ni mwakilishi wa utamaduni wa Kiislamu nchini humo.
Akizungumza mara tu baada ya kuteuliwa tena na idara ya uongozi ya baraza hilo kusimamia masuala ya baraza hilo, Musawi amesema kuwa baraza hilo sio mwakilishi wa moja kwa moja wa kila jambo la Waislamu wa Ufaransa bali ni mwakilishi wao kuhusiana na masuala ya kiutamaduni. Amesema kuwa kutokana na kuwa baraza hilo linawajumuisha Waislamu walio na uraia wa nchi tofauti, shughuli na matakwa yake pia yanaakisi matakwa ya Waislamu wote wanaoishi nchini Ufaransa. Akijibu tuhuma kwamba baraza hilo linajishughulisha zaidi na masuala ya wahajiri Waislamu wa Morocco, Musawi amesema kwamba tuhuma hizo hazina msingi wowote kwa sababu amekuwa akiungwa mkono na Waislamu wote wakiwemo wa Algeria ambao ndio wanaoendesha shughuli za msikiti mkuu wa Paris.
Ni muhimu kuashiria hapa kwamba Baraza la Waislamu la Ufaransa ni kiunganishi muhimu kati ya jamii ya Waislamu na serikali ya nchi hiyo. Wanachama wa idara ya uongozi ya baraza hilo huchaguliwa kupitia uchaguzi mkuu ambao hufanyika katika maeneo tofauti ya Ufaransa na kisha wanachama wake kumchagua kiongozi mkuu wa baraza hilo. 812856
captcha