IQNA

ISESCO kuhudhuria kikao cha mawaziri wa nje wa nchi za Kiislamu

16:30 - June 26, 2011
Habari ID: 2144709
Abdul Aziz Othman at-Tuweijri, Katibu Mkuu wa Shirika la Elimu Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO anatazamiwa kushiriki katika kikao kitakachofanyika hivi karibuni cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama.
Kikao cha 80 cha mawaziri hao kimepangwa kufanyika kuanzia tarehe 28 hadi 30 za mwezi huu wa Juni katika mji wa Astana ambao ni mji mkuu wa Kazakhstan.
Katika kikao hicho at-Tuweijri atazungumzia masuala ya kuimarisha jamii ya Kiislamu katika mazingira hivi sasa yanayotawala katika ulimwengu wa Kiislamu.
Katibu Mkuu wa ISESCO pia anatazamiwa kutoa ripoti kuhusiana na shughuli za shirika la ISESCO kwa msingi wa ratiba ya miaka 10 ya Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC.
Katika kikao cha Astana washiriki wa kikao hicho watachunguza mipango ya shirika hilo ya kuimarisha mazungumzo ya tamaduni mbalimbali na njia za kukabiliana na fikra na mitazamo potofu kuhusiana na mafundisho ya Kiislamu katika nchi za Magharibi. 814879
captcha