IQNA

Mwanamke bora muhubiri wa Uislamu kuarifishwa Malaysia

16:25 - June 26, 2011
Habari ID: 2144711
Baada ya kuchaguliwa imam bora wa swala ya jamaa kupitia kipindi kimoja cha televisheni nchini Malaysia, televisheni nyingine binafsi ya nchi hiyo ina mpango wa kuandaa kipindi kingine cha kuchagua mwanamke bora zaidi anayehubiri Uislamu nchini humo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Ajib, televisheni ya al-Hijrat inapanga kuendesha kipindi cha Sulha kwa ajili ya kuchagua mwanamke huyo bora.
Kipindi hicho ambacho kitaanza kurushwa hewani mwishoni mwa mwezi Oktoba kitakuwa katika sehemu 13 ambapo wanawake wa Malaysia wanaohusika na masuala ya kuhubiri Uislamu watashirikishwa na mbora kati yao kuchaguliwa.
Lengo la kuandaliwa kipindi hicho limetajwa kuwa ni kuarifisha nafasi muhimu ya wanawake katika uzingatiwaji wa misingi na mafundisho ya Kiislamu. 815262

captcha