IQNA

Baraza la Waislamu Ufaransa lawataka Wafaransa kuonyesho mshikamano wao na Wasomali

15:50 - August 02, 2011
Habari ID: 2164132
Mwenyekiti wa Baraza la Waislamu la Ufaransa (CFCM) Muhammad Mussawi amewataka Waislamu wa nchi hiyo kuonyesha mshikamano wao na wananchi walioathiriwa na baa la njaa wa Somalia.
Mussawi amewataka Waislamu wa Ufaransa kushirikiana na jumuiya za kiraia kwa ajili ya kutuma misaada yao ya kibinadamu katika nchi zilizoathiriwa na njaa za Afrika.
Amesema mshikamano na kutoa misaada kwa waathirika kunapaswa kuwa nara ya Waislamu wote katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani na kwamba Waislamu wa Ufaransa wanapaswa kufanya juhudi za kuokoa maisha ya Wasomali na watu wengine waliokumbwa na baa la njaa katika nchi za Kiafrika.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu Ekmeleddin Ihsanoglu pia ametoa wito kama huo akiwataka Waislamu kukabidhi misaada yao kwa jumuiya za misaada ya kibinadamu kwa ajili ya watu walioathiriwa na njaa huko Somalia. 836116

captcha