Ayatullah Sheikh Issa Qasim aliyasema hayo jana katika hotuba za Sala ya Ijumaa mjini Manama. Ameashiria matakwa ya wananchi na akasema wananchi hawawezi kustahamili hatua yoyote ya kupuuzwa matakwa yao.
Amezungumzia ubaguzi unaofanyika katika jamii ya Bahrain na kuongeza kuwa wahatavumilia kucheleweshwa marekebisho wa kudumishwa ufisadi na hali mbaya.
Sheikh Issa Qasim aneashiria adhabu za vfungo zilizotolewa dhidi ya maelfu ya wananchi wa Bahrain na kufukuzwa wengine katika idara za serikali na amelaani hatua ya serikali ya kuwafukuza watu makazini na kuwatesa kwa njaa makumi ya maelfu ya wanawake, watoto wadogo na watu wazima kwa tuhuma ya kushiriki katika maandamano au mikutano na kuajiri wageni na kuwapa mishara ya juu.
Ayatullah Qasim amekosoa pia utendaji wa nchi za Magharibi kuhusu kadhia ya Bahrain na akahoji Marekani na Ulaya wanamhami na kumtetea nani? Amesema nchi hizo za Magharibi zinatafuta vibaraka na watumwa ili waweze kupora utajiri wa mataifa mbalimbali, kudhibiti maeneo muhimu ya kijiografia na kuwakoloni watu.
Amesisitiza kuwa nchi za Magharibi na madola ya kibeberu yanaziunga mkono tawala tegemezi kwao na tawala zinawapa utajiri na mali ya wananchi.
Ayatullah Issa Qasim ameeleza kushangazwa na hatua ya utawala wa kifalme wa Bahrain ya kuwafukuza wanafunzi katika vyuo vikuu na kulaani kitendo hicho. 837755