IQNA

Sadiq al Jamri:

Mapinduzi ya wananchi wa Misri yatalindwa kwa kuwatimua wafuasi wa Marekani katika jeshi la nchi hiyo

14:50 - August 07, 2011
Habari ID: 2166622
Jeshi la Misri limekuwa chini ya udhibiti wa Marekani kwa zaidi ya kipindi cha miaka 30 na iwapo Baraza Kuu la Kijeshi la Nchi hiyo linataka kufanikisha mapinduzi ya wananchi halina budi kulisafisha jeshi la chi hiyo kwa kuwatimua wafuasi wa Marekani.
Hayo yamesemwa na Sadiq al Jamri ambaye ni miongoni mwa wanachama wa mapinduzi ya Februari 14 nchini Bahrain. Al Jamri ameiambia IQNA kwamba jeshi la Misri limekuwa likilipwa na Marekani kwa zaidi ya miaka 30 na kwa msingi huo vijana wa Mapinduzi ya Januari 25 na vyama vya siasa vinapaswa kutambua kwamba ili kuweze kulinda mapinduzi hayo yasiporwe na wageni hususan Marekani, Baraza Kuu la Kijeshi linalotawala Misri linalazimika kulisafisha jeshi na kuwatimua wafuasi wa Marekani na utawala ghasibu wa Israel.
Amesema Marekani inataka kuteka mapinduzi ya wananchi wa Misri kwa msingi huo inatumia njia ya kutoa fedha kwa jumuiya na asasi za kiraia za Misri kwa kisingizio cha kuimarisha demokrasia. Ameongeza kuwa fedha hizo zinazotolewa pia kwa asasi za kiraia nchini Tunisia zinatolewa kwa lengo la kuteka mapinduzi ya wananchi na kulea majasusi watakaokabiliana na harakati za wananchi na hatimaye kupotosha malengo ya mapinduzi hayo.
838408
captcha