IQNA

Ikhwanul Muslimin yafanya uchaguzi wa kwanza wa wazi

17:15 - August 07, 2011
Habari ID: 2166690
Harakati ya Ikhwanul Muslimin ya nchini Misri imefanya uchaguzi wake wa kwanza wa wazi tokea kuasisiwa harakati hiyo, ikiwa ni katika juhudi za kuwachagua viongozi wake wa ngazi za juu.
Uchaguzi huo ulifanyika hapo jana Jumamosi alasiri ikiwa ni moja ya ishara za kuruhusiwa kiwango fulani cha uhuru wa kisiasa na demokrasia tokea wakati wa mapinduzi ya wananchi yaliyofanyika tarehe 25 Januari.
Wamisri waliowengi wamefurahishwa na uchaguzi huo wa kidemokrasia na wa wazi na kuongeza kuwa hayo ni matunda ya mapinduzi ya wananchi waliopigania uhuru wa kujieleza na shughuli za kisiasa.
Maafisa watatu watakaochaguliwa kupitia uchaguzi huo watashughulikia masuala ya uandamizi na utendaji wa harakati ya Ikhwanul Muslimin. 838759
captcha