IQNA

Uungaji mkono wa Iran kwa mapambano ni fahari kwa Hizbullah

14:30 - August 14, 2011
Habari ID: 2170213
Sheikh Naim Qassim, Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah amesisitiza kuwa tuhuma zinazotolewa dhidi ya harakati hiyo kuwa ni sehemu ya mradi wa pamoja wa Hamas, Jihad al-Islami, Syria na Iran, ni fahari kwa harakati hiyo ya mapambano.
Akizungumza hapo siku ya Ijumaa katika karamu ya iftari iliyoandaliwa kwa ajili ya kuunga mkono mapambano ya Lebanon, Sheikh Naim Qassim amesema kuwa jambo hilo halipasi kuhesabiwa kuwa ni tuhuma bali ni fahari kubwa kwa harakati hiyo. Amesema harakati ya Hizbullah haina adui yoyote ndani na nje ya Lebanon isipokuwa Israel na kwamba mvutano unaoonekana kati ya harakati hiyo na makundi ya ndani ya Leanon ni tofauti za kisiasa tu ambalo ni jambo la kawaida kabisa.
Sheikh Naim Qassim amesisitiza kwamba Harakati ya Mapambano ya Lebanon si kundi lenye silaha tu ambalo linaweza kufutwa bali ni mustkabali wa kila mwananchi wa Lebanon, ardhi, maisha na heshima ya taifa hilo, vitu ambavyo si rahisi kufutwa.
Amesema harakati hiyo ina malengo mawili muhimu ambayo ni kukomboa ardhi zinazokaliwa na utawala haramu wa Israer na kulinda zile zilizokombolewa kutoka kwa utawala huo. 842088
captcha