Akizungumzia suala hilo, Mr. Temitope Ashiwaju, Mkurugenzi wa Idara ya Uhusiano wa Umma ya shirika hilo amesema kwamba shirika hilo litakuwa likigawa chakula katika misikiti yote muhimu ya nchi hiyo katika mwezi wa Ramadhani. Amesema shirika hilo linazingatia sana umuhimu wa kuimarisha mawasiliano na wateja wake na kwamba mwezi wa Ramadhani umeliandalia fursa nzuri ya kuweza kushirikiana zaidi na wateja hao.
Kwa mujibu wa shirika hilo Baraza la Maimamu la Nigeria limeunga mkono mpango wa shirika hilo wa kutoa futari kwa Waislamu na kwamba wakuu wa misikiti ndio watakasimamia shughuli ya kugawa futari katika misikiti hiyo.842199