Filamu hiyo inatazamiwa kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya filamu nchini Iran.
Mtengeneza filamu mashuhuri wa Marekani Scott Anderson ambaye ameshinda zawadi ya Marekani ya Academy Award ametembelea sehemu ambazo filamu hiyo itatengenezewa katika maeneo ya kusini mwa Iran. Aidha wahusika wakuu katika utengenezaji filamu hiyo wamekutana ili kuandaa utekelezaji wa mradi huu mkubwa.
Anderson ambaye anatazamiwa kushiriki katika utengenezaji filamu hiyo amesema kuwa mandhari ya hujuma ya ndege dhidi ya jeshi la Abraha na kijiji cha wavuvi ni kati ya nukta ngumu za filamu hiyo ambazo zinahitajia utaalamu wa hali ya juu. Amesema filamu ya ‘Muhammad SAW’ itakuwa na nafasi muhimu sana katika kuinua kiwango cha sekta ya filamu nchini.
843499