IQNA

Bakhtiyar:

Wanawake wana nafasi muhimu katika maamuzi mbalimbali

15:03 - August 17, 2011
Habari ID: 2172736
Akiashiria mabadiliko ya kisiasa ambayo yametokea katika nchi za Kiislamu na kuwepo matabaka mbalimbali ya wananchi katika mabadiliko hayo, Nilufar Bakhtiyar, mbunge wa Pakistan amesema kuwa kuwepo wanawake katika mkondo mzima wa mabadiliko hayo kunathibitisha wazi nafasi yao muhimu katika maamuzi ya mabadiliko hayo.
Bakhtiyar ameyasema hayo alipokuwa akiyatembelea maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu mjini Tehran na kusifu mabadiliko hayo ya kisiasa kwa sababu yataleta mwamko wa Kiislamu duniani.
Amesema kuwepo kwa wingi wanawake katika harakati za mageuzi katika mataifa ya Kiislamu na Kiarabu kunabainisha hamu yao ya kuchangia mustakbali wa nchi hizo.
Akiashiria propaganda sumu na chafu za nchi za Magharibi dhidi ya wanawake wa Kiislamu, Bakhtiyar amesisitiza kwamba ushirikiano wa bega kwa bega wa wanawake wa Kiislamu katika harakati za kisiasa na kimapinduzi katika nchi za Kiarabu unabainisha wazi kulindwa haki zao katika nchi hizo.
Bakhtiyar amesema hata kama miaka mingi iliyopita mwanamke wa Kiislamu alikuwa akitazamwa kwa mtamo mbaya na kukandamizwa katika nchi za Asia, lakini mtazamo huo umebadilika taratibu na kwamba sasa wanawake wanaweza kujihusisha kwa uhuru kamili na masuala mbalimbali ya kisiasa na kijamii katika nchi zao bila kuwepo vikwazo vikubwa. 843618
captcha