IQNA

Mkutano wa Ubahai na Uzayuni wafanyika Tehran

12:54 - August 19, 2011
Habari ID: 2173373
Mkutano wa 'Ubahai na Uzayuni' ulifanyika jana mjini Tehran katika maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani.
Mkutano huo ambao ulijadili uhusiano wa Ubahai na Uzayuni ulihutubiwa na Hujjatul Islam Walmuslimin Mahmoud Ridhaa Qasimi ambaye amefafanua historia fupi ya Ubahai na uhusiano wake na madola ya kikoloni. Amesema kuwa moja ya sheria za Ubahai ni kuruhusu ndoa kati ya maharimu na kudai kwamba kuna Mtume mwingine liyekuja baada ya Nabii Muhammad SAW licha ya Qur'ani kusisitiza kuwa Muhammad SAW ndiye Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu.
Makao makuu ya Baraza Kuu la Mabahai lenye wanachama 9 liko huko Israel na linapewa himaya na misaada na utawala huo ghasibu. 845935
captcha