Kikao hicho ambacho kilifanyika jana jioni kimehutubiwa na mkuu wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu la Iran Muhammad Baqir Khurramshad. Kikao hicho kimehudhuriwa na wadau wa masuala ya Qur'ani, wasomi na watafiti wa sayansi ya Qur'ani.
Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur'ani yaliyoanza tarehe 28 Julai hapa mjini Tehran yataendelea hadi 26 Agosti. 845923