IQNA

Siku ya kuawa shahidi Imam Ali (as) kuwa siku ya mapumziko Najaf

12:22 - August 20, 2011
Habari ID: 2173767
Baraza la ugavana wa mji mtakatifu wa Najaf nchini Iraq limetangaza kwamba siku ya Jumatatu tarehe 21 Ramadhani inayosadifiana na tarehe 22 Agosti ambayo ni siku ya kuuawa shahidi Imam Ali bin Abi Twalib (as) itakuwa siku ya mapunziko rasmi mjini humo.
Limesema kuwa mbali na vituo vya usalama, afya na huduma za dharura kwa ajili ya wafanyaziara, idara zote za mji huo zitafungwa kwa ajili ya kuheshimu siku hiyo ya maombolezo kutokana na kifo cha mtukufu huyo wa Nyumba ya Mtume (saw).
Mkuu wa idara ya upashaji habari ya baraza hilo amesema kwamba kwa mujibu wa maamuzi ya baraza hilo, idara zote zinazosimamia masuala ya ulinzi, afya na usalama pamoja na huduma kwa ajili ya wafanyaziara zitatakiwa kuendesha shughuli zao kama kawaida katika siku hiyo ya maombolezo. 846129
captcha