Gazeti la Darul Hayat limemnukuu msemaji wa harakati ya wanamapinduzi wa Libya Ahmad Umar Bani akisema kuwa Jalud aliondoka jana mjini Tripoli na kujiunga na wanamapinduzi wa nchi hiyo.
Hata hivyo Ahmad Umar amekataa kuweka wazi mahala alipo aliyekuwa kiongozi nambari mbili wa utawala wa Gaddafi kutokana na masuala ya kiusalama.
Vyombo vya kuaminika vimeripoti kwa Abdulsalam Jalud alifanikiwa kuondoka jana mjini Tripoli akiwa pamoja na familia yake na kujisalimisha kwa wanamapinduzi wa Libya katika mji wa Zintan ulioko magharibi mwa mji mkuu.
Wapiganaji wanaopinga utawala wa kidikteta wa Libya wanaendelea kusonga mbele kuelekea Tripoli, makao makuu ya dikteta wa nchi hiyo Muammar Gaddafi. 846577