IQNA

Mapinduzi ya eneo, fursa ya kuondolewa hitilafu za kimadhehebu

15:05 - August 21, 2011
Habari ID: 2174482
Mapinduzi yanayoendelea katika Mashariki ya Kati na kaskazini mwa bara la Afrika ni fursa nzuri ya kuwekwa kando tofauti za kimadhehebu na kikabila kati ya Waislamu.
Kwa kuwekwa pembeni hitilafu hizo Waislamu wanaweza kushirikiana vyema na kujirejeshea heshima iliyopotea miaka mingi iliyopita.
Hayo yamesemwa na Fat'hi al-Ghazwani Mkuu wa Umoja wa Vyama vya Wanachuo wa Tunisia ambao ni Tawi la Vijana la Chama cha an-Nahdha cha Kiislamu nchini humo.
Akizungumza jana katika kitengo cha wanachuo katika maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani mjini Tehran, al-Ghazawani amesema kuwa Mwenyezi Mungu daima anawasihi waja wake katika Qur'ani Tukufu kuwa na umoja na mshikamano kwa sababu jambo hilo bila shaka linadhihirisha nguvu na uwezo wao mkubwa katika kupambana na mifarakano na udhaifu. Amesema hayo ni matunda makubwa waliyoletewa watu wa mataifa mbalimbali na Mitume wao. Ameendelea kusema kuwa Uislamu ambayo ni dini ya mwisho ya Mwenyezi Mungu kwa wanadamu inayataka mataifa na makabila yote kuungana katika umoja na kupwekesha Munga Muumba. 846985
captcha