Huku uhusiano wa Misri na Israel ukiendelea kuharibika, kijana mmoja mwanamapinduzi wa Misri ameteremsha chini na kuichoma moto bendera ya Israel katika ubalozi wa utawala huo nchini Misri, na kuweka bendera ya Misri mahala pake.
Sambamba na kuendelea maandamano ya wananchi wenye hasira wa Misri mbele ya ubalozi wa Israel mjini Cairo hii leo, kijana Ahmad Shahat jana alipanda katika jengo la ubalozi huo na kuteremsha chini bendera ya Israel. Kitendo hicho kilifuatiwa na nderemo na vifijo vya watu huku waandamanaji wakiwazuia polisi kumkamata kijana huyo.
Wananchi wa Misri wamekuwa wakiandamana kwa siku ya tatu leo kutaka balozi wa Israel afukuzwe nchi kwao kutokana na kuuawa askari polisi watano wa Misri na jeshi la Israel katika mpaka wa pande mbili siku ya Alkhamisi.
Maandamano hayo yameendelea licha ya Ehud Barack Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni kuiomba Misri msamaha hapo jana kutokana na mauaji hayo. 847235