IQNA

Ayatullah Khatami:

Kadhia ya Palestina ni suala la Waislamu wote

21:40 - August 26, 2011
Habari ID: 2177077
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa moja ya ujumbe muhimu za mwamko wa Kiislamu katika Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika ni kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel unajitayarisha kwa ajili ya kutoweka.
Ameongeza kuwa baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran hapo mwaka 1979 ulianza mwenendo wa kudhalilika utawala bandia wa Israel. Ayatullah Ahmad Khatami amesema kuwa kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran Israel ilikuwa bwana wa Mashariki ya Kati lakini baada ya mapinduzi hayo kulianza mapambano ya Intifadha ambayo yameunyima usingizi utawala ghasibu wa Israel uliolazimika kutupilia mbali fikra ya kuasisi "Israel Kuu" yenye mipaka ya kuanza Mto Nile hadi Euphrates.
Khatibu wa Sala ya Ijuma ya Tehran amesema baada ya hayati Imam Khomeini kutangaza Ijuma ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Quds, suala la Palestina lilitangazwa tena kama kadhia kuu ya ulimwengu wa Kiislamu, ilhali hapo awali zilifanyika juhudi za kulidhihirisha suala hilo kuwa ni la Kiarabu na linalowahusu Waarabu peke yao.
Ayatullah Khatami amesema kuwa mwamko wa sasa wa Kiislamu ni tukio lisilokuwa na kifani katika historia. Ameashiria siku chungu na zilizojaa madhila za dikteta wa Libya Kanali Muammar Gaddafi baada ya kuitawala nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 40 na akasema kuwa kiongozi huyo alikuwa dhalili na duni mbele ya Wamagharibi licha ya kujifanya fisi na chui kwa wananchi wake. Vilevile amewausia wanamapinduzi wa Libya kuwa macho mbele ya njama za nchi za Magharibi hususan Marekani na kulinda umoja na mshikamano wao katika kuijenga upya nchi hiyo kutokana na uharibifu wa miongo minne ya utawala wa Gaddafi na mashambulizi ya majeshi ya NATO.
Hatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran pia amewashukuru Wairani kwa ukarimu wao katika kuwasaidia Waislamu wenzao wa Somalia na akawahimiza kutoa misaada zaidi kwa waathirika wa baa la njaa huko Somalia. 850002

captcha