IQNA

Mawahabi wa Saudia watoa fatuwa ya kuuawa Wairaq

18:56 - August 28, 2011
Habari ID: 2178264
Ali al Adiib ambaye ni miongoni mwa maafisa wa chama cha Kiislamu cha al Daawa cha Iraq amesema kuwa Mawahabi wa Saudi Arabia wametoa fatuwa inayohalalisha mauaji dhidi ya raia wa Iraq na kueneza gaidi nchini humo.
Ali al Adiib amesema, makundi yenye misimamo mikali ya Kiwahabi na kisalafi yanaendesha shughuli zao katika maeneo mbalimbali ya Iraq.
Al Adiib ameyasema hayo katika kongamano la "Mchango wa Maulamaa wa Dini katika Kufanikisha Mapatano ya Kiaifa" linalofanyika mjini Baghdad.
Amesema kuwa katika baadhi ya vyuo vikuu vya Iraq kunatolewa darsa na mafunzo ya kisalafi na Kiwahabi yanayowakufurisha baadhi ya Waislamu.
Mbunge huyo wa Iraq amesema kuwa maulamaa wa Kishia na Kisuni wa Iraq miaka kadhaa iliyopita walifunga mkataba wa Makka chini ya usimamizi wa serikali ya Saudi Arabia kwa ajili ya kuzuia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Iraq na kuimarisha umoja na mshikamano wa Kiislamu.
Ali al Adiib amesisitiza kuwa maulamaa wa kidini wanapaswa kuwa na nafasi muhimu katika utekelezaji wa mkataba huo.
Afisa huyo wa chama cha Daawa amesema baada ya kuondolewa madarakani utawala wa Saddam Hussein, baadhi ya viongozi wa Iraq wamekuwa wakisisitiza kuwa baadhi ya nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi zinawapa hifadhi na kuyasaidia makundi ya kigaidi ya Kiwahabi na kufadhili makundi hayo kwa fedha na silaha kwa shabaha ya kufanya mashambulizi ya kigaidi nchini Iraq. 851086

captcha